Hello Everyday Mbeya!

Who doesn’t like a good road trip? Now let’s turn the journey into the best bit of your experience by following these incredible routes while in Mbeya.


Mount Rungwe Nature Reserve

Vipo vitu vizuri kuhusiana na safari za barabarani, hata kwa mguu katika mandhari tele unaweza kupata the best out of them, lakini leo nakuletea maeneo ambayo yatakushangaza kwa kupita na gari lako.

Kawetire, Mbeya/Chunya


Kawetire (Chunya Road)

Kilomita 31 pekee kutoka Mbeya mjini katika barabara iendayo wilaya maarufu kwa uchimbaji wa madini (Chunya) utakutana na barabara hii yenye kona za kushangaza katika eneo liitwalo Kawetire (Kawetere). Barabara hii iliyo katika muinuko wa juu inapambwa nakshi za bonde la Ufa na kuifanya kuwa sehemu ya kivutio kikubwa.

Inashangaza namna ambazo kilomita hizi sabini kutoka Mbeya Town hadi wilayani Chunya zilivyobadilika kutoka kuwa ‘karaha’ hadi ‘raha’, siku za awali kabla ya ujenzi wa barabara hii ya kisasa, iligharimu zaidi ya masaa manne kusafiri kati ya sehemu hizo mbili kutokana na ubovu wa miundombinu.

Kwa sasa imekua sehemu nzuri kwa road trips na ukipita wakati wa foggy unaweza kusahau kuwa upo Bongoland!


Muonekano wa bonde la Ufa


Kona ya wilaya na kona ya mkoa 🙂 🙂

Unaweza kwenda wikiendi kwa ajili ya mapumziko katika eneo lililo pembezoni mwa barabara hii maarufu kama ‘viewpoint’. Hii ni sehemu mahususi kwa jailli yako kutazama bonde la Ufa na ndio sehemu pekee duniani unaweza kutazama bonde hilo katika pande tatu.


Baadhi ya maeneo katika barabara hii ni picha inayosubiri kupigwa, basi na ushuke ujipatie silhouette hizi za kuvutia.

Kikusya, Ipinda, Matema (Matema/Kyela)


Fikiria barabara hii 🙂 🙂 🙂

Barabara ya Kikusya ina kila picha kwa msafiri, kuanzia mashamba ya mpunga, michikichi na kokoa zilizo pembezoni mwa barabara hii ya kilomita 46, madaraja, milima ya livingstone na harufu murua ya mchele wa Kyela uliopo shambani. What more can you ask?

Sasa kama haitoshi, fikiria mito inayokatisha chini ya madaraja kwenda kulijaza ziwa Nyasa, na sasa hebu tafakari kuhusu ziwa Nyasa lenyewe.


Livingstone Mountain


Lake Nyasa


Safu za milima ya Livingstone

Kinachofanya Matema Beach iwe spesheli ni hizi safu za milima ya Livingstone, uwepo wa ziwa pembezoni mwa milima hii kunafanya road-trip kati ya Matema na Kikusya ziwe moto sana.

Sasa utaachaje kusimama na kujipatia kapicha?

There’s something romantic about hitting the open road, free of the constraints of schedules, agendas and itineraries.  A road trip offers the chance to see the world with the added flexibility of pitstops wherever and whenever you want – to grab the perfect picture, or sample local culture, at your own pace. -Unknown

Ushirika to Ibanda (Kyela)

Everyone’s heard of Mashamba ya Chai, lakini ni nini kinayafanya yawashangaze watu? Unaweza usizingatie uzuri wa maumbile ya mashamba ya chai katika barabara inayotoka Ushirika hadi makutano ya Ibanda, lakini ukijaribu kidogo tu kushuka na kutazama nje au kupapasa macho yako kupitia vioo vya gari lako utashangazwa na uzuri wa nchi yetu.

Barabara hii iko na the best that nature can throw at you, so this is one road trip you should try to do as soon as you get the chance. And savour every moment.

Igawilo (Mbeya)

Yako maeneo mawili muhimu kwa kutazama jiji kutokea juu, ukiacha barabara itokayo Chunya kuingia Mbeya mjini, nimechagua barabara hii kwa sababu ya the scenic Mbeya ranges. Hebu tazama Muonekano wa safu za milima ya Mbeya, how about it!

Pita hapa usiku na ujionee mataa ya nchi yanavyopendezesha jiji letu.

 


Isyonje

Ukienda juu kidogo kutoka Igawilo upo mji mdogo maarufu uitwao Isyonje. Mji huu ulio katika muinuko mkubwa unarekodi halijoto ndogo zaidi kwa maeneo yaliyo jirani na Mbeya mjini, na baridi yake hufanya muonekano wa barabara ufichwe (visibility).

For many seasoned drivers, this is regarded as one of the best, and most beautiful places to drive.

-Eric Muganga

Tukuyu to Katumba (Tukuyu)

Nani asiyependa milima?


Mount Rungwe View

Si lazima upande mlima Rungwe ili uweze kufurahia mandhari hii, as you drive along kutokea Mjini Tukuyu kuelekea Katumba utakutana na viewpoints hizi nzuri za mlima Rungwe. Fahamu kuwa mlima huu ni wa tatu kwa ukubwa hapa nchini.

Uwepo wa mlima Rungwe umefanya maeneo mengi ya Rungwe hasa kutoka Kiwira hadi Tukuyu kuwa na mito mingi inayotiririsha maji yake, na mito hiyo imetengeneza scenery za kushangaza.

Shuka upate picha Nyengo!

Mlima Mbeya na Loleza (Mbeya Town)

Pasina shaka safu hizi za milima ndio Kilimanjaro ya nyanda za juu kusini, na licha ya kuwa utahitaji a serious 4×4 kuzitawala safu zake kwa gari bado uzuri wake hauchoshi. Sasa ni nani atapeleka 4×4 yake mlimani?


Juu ya mlima Loleza

One of the best places za kutazama dusk (moment after sunsets) ni hapa kileleni Loleza, fikiria kuwa juu ya mlima walau mita 2656 juu ya usawa wa bahari na ku-jikabidhi katika hali hii?

Kitulo National Park au Bhujonde Beach ni mojawapo ya sehemu zinazotupa muonekano maridadi wa jua linalozama -lakini ukiwa juu ya kilele cha Loleza ni zaidi ya uzuri 🙂 🙂 🙂


Iziwa

As you drive to the top of Loleza kwa kutumia njia ya Iziwa zipo mandhari tele za kushangaza sana, hapa ni juu kidogo ya Iziwa unapopandisha Loleza, sasa muonekano wa jua linalozama ukiwa hapo Iziwa na nakshi pambe za mlima Mbeya ni zawadi kwako na gari lako. Kwanini usishuke ujipatie kapicha?

Ifisi (Mbalizi)

Ushawahi kufikiria kuwa Mbalizi patafaa usimame na kupiga picha? Au tuseme ushuke na kutazama nje?
Well, nimekukusanyia picha tatu tu ambazo zitakupa kila sababu ya kukanyaga break za gari yako na kushushua kioo chako.


Ifisi Game-view Hotel na Ravine (zoo)


Daraja la reli ya Tazara na mji wa Mbalizi


Flyover ‘flani’ Malafyale 🙂 🙂 🙂 🙂


Safu za milima ya Mbeya kutokea Songwe na Muonekano wa uwanja wa ndege


Songwe International Airport

Uporoto (Mbeya)

Milima ya Uporoto ni mojawapo ya vilele vinavyofanya mji wa Mbeya uvutie na hapa zipo njia zinazoelekea ziwa Ngosi lililopo katika msitu wa Uporoto. Njia hizi zinaanza kupoteza u’scenic wake kutokana na maboresho ya barabara zake lakini bado haziachi asili yake. Hii ndiyo sababu nimekukusanyia the best of Iduda route as you drive to the Poroto ridge.


Nani hapendi adventure!


Kaanga Selfie… Ekotite 🙂 🙂


Sasa usiende mwenyewe, nenda na wenzako

Ukiwa juu ya safu za milima ya Uporoto unapata nafasi za kutazama jiji lako pendwa.

Yapo maeneo mengi mazuri ya wewe kuendesha gari lako na kujipatia the best out of nature, sitoweza kukuonesha yote lakini walau hayo juu yatakuvutia kwenda kituo cha mafuta na kuu-anza mwendo.

Hapa chini nakupa dodoso la maeneo mengine unayoweza kufurahia uzuri wake as you drive

Kitulo (Makete/Njombe)

Hebu tazama uzuri wa Kitulo…

Igawa (Mbeya)

Kapunga Rice Farm Project Ltd (Mbarali/Chimala)

Lake Kisiba (Masoko/Tukuyu)


Im not so sure if it is still applicable to drive around the lake these days, laking kama unaweza Hebu jaribu

Shamba la Miti kiwira (Kiwira)

So these are places nimekukusanyia leo, na kumbuka kuwa sehemu hizi si vizuri kwenda peke yako.

Zipo scenic route za boti juu ya ziwa Nyasa, basi wakati ujao nitakuonesha namna gani sailing above this lake ni spesheli; na tutaanzia Matema, Liyuli hadi huko Mbamba Bay.

Iwapo umeishachukua route walau tatu katika hizi, nenda sasa hive pale Utengule Coffee Lodge Mbalizi na ujiagizie kitu hiki hapa chini; ukifika pale waambie Shah amekuagiza 🙂 🙂 🙂 and that you are willing to pay on cash by yourself.


And just before I go… where is this place on earth?

 

Video: Tazama Kalambo Falls kwa ufupi

Wasalaam,

Makala hii imeandikwa na Shah Mjanja.

Shah Mjanja ni mpiga picha wa muda mrefu, muandishi na mtayarishaji wa makala za televisheni na filamu, mhifadhi, mwanamuziki na msafiri. Shah Mjanja ni muanzilishi wa Everyday Mbeya na Studio Native.

Shah Mjanja ni Ofisa wa Habari za klabu ya Mbeya City FC.

Mawasiliano:

Simu: +255-682-326410
Barua Pepe: shah@everydaymbeya.com

Work Address
Posta House, FL
Posta Street/Lupaway road
Box 312
Mbeya Town