Salaam,
Ninayo furaha kuwaeleza kuhusu program yetu ya redioni itakayoanza kuruka wiki hii kupitia Access FM (100.9) katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Njombe, Iringa, Singida na Tabora.
Program hii ya redio inaitwa Everyday Mbeya na itaruka hewani kila siku ya jumamosi saa kumi na mbili jioni hadi saa moja jioni na kila siku ya jumapili saa nane mchana hadi saa tisa mchana.
Program hii ni sehemu mojawapo ya mipangilio yetu ya kutangaza utalii kusini mwa Tanzania na hasa zaidi mkoa wa Mbeya.
Program itaangazia zaidi taarifa za kitalii, maoni, uchambuzi na mipangilio ya safari za kitalii.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu kipindi hiki cha redio kupitia www.everydaymbeya.com/radio
Kwa namna ya pekee naishukuru timu yetu katika EverydayMbeya kwa kuunganisha rasilimali zote hadi kufanikisha kipindi hiki, lakini pia mkurugenzi na staff wa Access FM kwa ushirika ulio tukuka.
Imetolewa na
Shah Mjanja
Mhifadhi —Everyday Mbeya
Office
Posta House, FL
02 Mtaa wa Posta
53100 Mbeya