Hadi mwaka 1920, hapakuwa na mji unaoitwa Mbeya…
Kulikuwa tu na eneo ambalo Wasafwa walikuwa wanachimba chumvi (ibheya) at the bed of Mount Loreza…
Miaka michache baadaye Wahindi wa South Africa wakawa so interested na dhahabu ya Lupa (kwa marejeo ya geological map as it was drawn by Germans)
Waakaanza kufika kwa wingi eneo ambalo Wasafwa walianza kuliita Ibheya (kwenye chumvi) wakiwa njiani kwenda Lupa…
Kwa sababu eneo hili halikuwa na huduma muhimu kama malazi, Wahindi na wazungu wachache wakaanza kuweka mahema wakiwa njiani kwenda Lupa (ndiyo sababu ile barabara kuanzia Jakaranda – Idas pub hadi nyumbani kwa mkuu wa Mkoa inaitwa Lupa Way).
Hivyo, Lupa Way (basically ilipo soko lililoungua hadi Posta) ndipo yakawekwa mahema na Wahindi na Wazungu hao
Hadi mwaka 1927, Wahindi wakapafanya Lupa Way malazi yao ya kuduma…. Na wakashindwa kutamka Ibheya, wakaita Mbeya….
Hivyo, pakaanza kukua kwa kasi kubwa sana….
Serikali ya kikoloni ya Uingereza ikaamua kubuni rasmi mji…
Ikaupa zone tatu…
Zone ya kwanza Government street (Uzunguni), zone ya pili Sokomatola (kwa Waswahili) na zone ya tatu Lupa Way (kwa Wahindi).
Kutoka 1927 – 1939 Vita ya kwanza ya dunia ilipoibuka, Mbeya ikakua kwa kasi kwa sababu ya biashara ya dhahabu ya Wahindi..
Ikachochewa na uwepo wa Great North Road…
1939 – 1960 Mbeya ikapata umaarufu zaidi na kukua kwa sababu ya harakati za kupigania uhuru. Ikawa hub ya wapigania uhuru wa Malawi, Zambia, Zimbabwe, Namibia na South Africa….
1960 – 1975 Mbeya ikaongezeka kasi ya kukua kwa sababu ya kuwa lango la kusini (South Corridor) hususani katika kipindi ambacho Kusini inapambana kupatikana kwa uhuru wa Zimbabwe, Namibia, Angola na Afrika Kusini.
1975 – 1995 Kukua kwa Mbeya kukachochewa zaidi na kujengwa kwa kituo kikubwa cha pili kwa Tanzania kwenye reli ya Tazara… Na vilevile, mwanzoni mwa 1990 Wamarekani walipojenga karakana ya reli ya kisasa zaidi (ya pili kwa ubora Kusini mwa jangwa la Sahara – ikizidiwa na Afrika Kusini tu)
Mbeya ikawa hub ya viwanda eneo lote la nyanda za juu kusini. Viwanda vingi vilijengwa kipindi hiki na kasi ya ukuaji wa mji wa Mbeya ilikuwa kubwa sana.
Kukawa na kampuni kubwa ya umma ya ujenzi MECCO (Mwananchi Engineering and Construction Company).
Kukaibuka na timu nyingi zenye soka la maana kama Mecco, Tazara Rangers na Tukuyu Stars.
Na ndicho kipindi Songwe International Airport ilidizainiwa (ikaja kujengwa miaka 30 baadaye 😳)
1995 – 2005 Maendeleo ya Mbeya yakaanza kudorora kwa kasi… Mbeya ni miongoni mwa mikoa ya mwanzo kupokea mageuzi ya vyama vingi… Ndicho kipindi viwanda vilikufa. Kiwanda cha nguo, kiwanda cha zana za kilimo, kiwanda cha saruji (kikainuka baada ya uwekezaji) kiwanda cha sabuni – Hisoap, ranchi ya taifa nk.
Timu mpya ya Tiger ya Tunduma ikaibuka.
1 Julai 2005 Mbeya ikapata rasmi hadhi ya jiji
2005 – 2015 Mbeya ikaanza kuinuka taratibu sana. Taasisi za elimu ya juu, makampuni ya simu na sekta ya fedha vikaanza kuhuisha tena uchumi wa Mbeya.
Lakini, siasa ikaendelea kuzorotesha…
2015 – sasa…. Hali ndo kama mnavyoiona…
Nimejaribu kuandika harakaharaka kila ninachokumbuka kichwani… Lakini ni mengi zaidi ya haya… Nikitulia, ntasimulia.
Abdul
Well written! Kudos kwa Fadhy Mtanga. This should be added kwenye page ya Mbeya kwa Wikipedia. Kazi nzuri wazee!
Mjanja Shah
Man, asante sana. We moving forward!
Stewart Ngwale
Lupa way ilikatishwa baada ya kuanzishwa miji hiyo mitatu na rasmi njia ya chunya kupitia isanga iganzo ilipoanza kutumika mpaka sasa imekuwa ndiyo njia rasmi, kukaibuka ujenzi holela kwa yeyote aliyekuwa na kipato alitamani kujenga na mji uliobuniwa ukawa ni jacaranda, old forest, majengo, ghana, block T na block Q huu ulijengwa na watu waliokuwa na kipato rasmi na maeneo makongwe ya Isanga, mabatini hii ilikuwa miji ya awali ya watu wasio na kipato rasmi
Kwanini isanga na mabatini? Hii ilikuwa ni maeneo ya karibu na mitaa yenye shughuli za uzalishaji.
Iyunga ilijawa na nyumba za wafanyakazi (kota) ambapo kila kiwanda kilikuwa na nyumba za wafanyakazi
Kipindi hicho kulikuwa na gari(basi) linalobeba wafanyakazi nakumbuka ZZK zana za kilimo walikuwa na usafiri wao unaowachukua wafanyakazi wao maeneo ya forest ya zamani juu ya viwanja vya sabasaba kuwapeleka makazini, pia kulikuwa na lile la kilimo uyole nadhani hili ndilo basi la mwisho kutumika kwani limedumu mpaka miaka hii ya 2010’s
Kukaibuka pia mabasi ya kiwanda cha saruji na. Cocacola ambayo yalikuja baada ya uchumi wa viwanda kuanza kuboreshwa upya miaka ya 2000’s
Steward
Mjanja Shah
Good stuff Dingi. Umetisha sana