Ilikuwa Tarehe 29/04/2017… Mida ya Saa Tisa alasiri… UnahisI hii picha ilipigwa kwa kifaa gan?… Simu au Drone camera au Kamera ile ya kawaida ulioizoea?
Hapo katika picha…Kuna maeneo mengi yanaonekana..na kwa mwenyeji wa Mbeya unaeza ukaZoom na ukatambua baadhi ya Maeneo..
Hii ni City Garden au Bustani Ya jiji la Mbeya ambayo ipo jirani kabisa na uwanja wa Michezo wa kumbukumbu ya Sokoine…
Hapo ilikuwa ni kipindi hii bustani bado ni mpya na watu ndo wanaanza kuifaham…
Nilikuwa nimebeba kamera yangu (Kamera Ya kawaida)..kwa lengo moja tu…kupiga picha za Mitaa ya Mbeya…
ila nilifika Mjini na kuliona jengo refu likiwa linajengwa na limefika mwsho ila walikuwa wanamalizia sehem za vyumba
Nilifika palee na kuwasalimu wale mafundi..ambao wanatumika kama vibarua tu..nikaongea na mmoja nikamwambia nahitaj kufika juu ya hili jengo..akasema nenda kaongee na Muhandisi mkuu yule pale…nikamwambia hapana..sio ishu kubwa…nataka tu nichek view..akasema sawaaa
Nilivyofika juu…nikamwambia nataka nipige picha akasema hapo ni ngumu Engineer akikuona itakuwa kesi yetu..nikamwambia picha nimesha piga tayr kichwan mwangu..ila nahitaj tu kutumia Kamera kwa Dak2..niitunze hii kumbukumbu ,,wala hakuna atakae ona wala kujua…alinipa ruhusa nikapiga picha hata kabla ya dak2 kuisha nikawa nimemaliza nikarudisha Kamera kwa begi..tukaanza kushuka ngazi
Wakati tunashuka akanambia ungejaribu tu kwenda kwa Engineer mkuu palee asingekuruhusu kufka huku…mana n hatari kwa jengo ambalo lipo kwenye matengenezo..nikamwambia nashukuru kwa kunipa ushirikiano japo n kwa njia za panya….
Nikajichek mfukoni nikaikuta buku (elf1 tu) nauli ya kurudi home..ila kwa jinsi nilivyofurah kupata hizii picha niliitoa kwa moyo mweupe nikampatia fundi nikamwambia utakula hata kyepeee ndugu yngu …..akashukuru sanaaa ,nikamwambia Mimi ndo natakiwa nikushukuru wewe sanaa
Nikaondoka na nikiwa na picha ambayo…
Niliipiga kwa dak 1 ,na kulipia ada ya shukrani ya elf1 tu..ila Thamani ya picha hii imekuwa kubwa kuliko hayo niliyoyapitia wakati naipata…
Kwa kifupi..hiyo ndo #PichaYaSiku toka kwa #JMson #KelvinJM…
#PichaYaDakika1 #PichaYaBuKu..
Makala haya yameandikwa na Kelvin JM
Kelvin ni mpiga picha mashuhuri jijini Mbeya, wa shughuli za harusi na matukio ya kitaalamu pamoja na safari.
Instagram: (@kelvin.jm)
Simu: +255687212281
Email: kelvin@everydaymbeya.com
Shah Mjanja
Picha ya Buku 😀😀😀, Hii ni bustani ya Jiji, ni eneo la wazi kwa wakaazi wa Jiji. Moja ya jukumu la halmashauri ni kuburudisha wakaazi wake, na bustani hii iliwekwa mahususi ili watu waende kustarehe na wenzao.
Kelvin asante sana kwa sharing.
Angel Malaika
I real love this place…. Kipindi hawajalifunga badoo… Nilikua nikipatwa na stress hii sehemu ilikua muhimu sanaa kwanguu kuondoa stressa.
Kuna siku nilikua na hasira sanaaa… nikasema ngoja nikake pale nipunguzee hasiraa.. nikakuta wamezungusha mabatii… Guess what??
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Sitakii kukumbukaaa
Raysa Ngelangela
Nimependa aliekuwa mkurugenzi wa jiji bwana amede mala baada ya kuona panashangaa shangaaa kawakabidhi tugimbe na babito watajua wao wafanye nini ili wakazi tupate starehe pale 👏 ndyo maana Kuna mabati bila Shaka kunajambo linaendelea
Stewart Ngwale
Kwa sasa kuna uwekezaji unaendelea pale, huenda kuna kigogo kachukua anataka kufanya ya tofauti
Tuombee afanye iliyo bora
Sirro Sirro
Ameshaeleza kwa uzuri kabisa jengo namna na thamani ya hii picha, ni picha ya buku tu toka NHIF tower I inaweza kukuondolea stress kwa kuiangalia tu. Kongole kwako Kaka JMson🤝👏
Sixtus
Shukrani kwa picha ya siku na maelezo mazuri kabisa 🙏