Hello Everyday, How are you all today!

So, the past weekend nimeenda Kitulo na nitapenda kushare kidogo taarifa za kitalii about kitulo, some of these stories nimeziweka @everydaymbeya huko Instagram, hopefully mlizitazama, na kama bado hufuatilii kurasa yetu please do it now!

Wote mnajua this is the season to Kitulo na hadi mwezi April bado inasemwa ni murua kwenda pale, Hivyo nitashare nanyi about five or six-to-know about Kitulo.

1. Njia
2. Viingilio
3. Malazi
4. Matarajio
5. Chakula
6. Activities

1. Njia

Zipo njia mbili mashuhuri, moja ni ile ya pale Chimala yenye wastani wa kilomita 110 hadi geti la hifadhi na njia ya pili ni ile ya Isyonje ambayo ina kilomita 88 hadi geti la hifadhi. Umbali naoutaja hapa ni kutokea Mbeya mjini.

Unaweza kwenda Kitulo kutokea Mkoa wa Njombe kupitia Makete, fahamu kuwa hifadhi hii kwa sehemu kubwa ipo Makete. Lakini Mbeya pana faida zaidi kutokana na kuwa na njia nyingi zaidi mfano Ndege, Reli na Barabara, plus kwa wasafiri na wageni, mkoa wa Mbeya una activities tele, kwa hiyo apart from Kitulo basi unaweza pia kuona mengine mengi mfano vilele,  maporomoko ya maji na mengine mengi.

Safari yangu ya Mrisho nilipita Chimala, njia hii ina sceneries bora zaidi hasa za muonekano wa eneo chepe la bonde la Ihefu na Usangu, kilimo chake cha mpunga na kona zinazovutia na kutisha. Challenge ya njia hii ni zile kona zake kali. Pana kona takribani 36 katika muinuko mkali, na utahitaji gari imara yenye service nzuri, unless otherwise utaishia njiani.

Njia hii ina kilomita 24 kutokea pale Chimala kwenda Matamba kijiji kilicho jirani na hifadhi ya Kitulo. Inaogofya sana njia hii na kama una homa ya mlima usiende nayo.

Njiani pana miti ya asili mingi na upepo mzuri, kama una facilities basi unaweza park na kula snacks


-Tunachimba Dawa 🙂 🙂

2. Viingilio

Viingilio hifadhini ni nafuu sana kwa mswahili, utalipa 5,000/- Tshs ambayo ukiweka VAT jumla itakua 5,900/- Tshs. Kwa sasa mtu mzima. Gari isiyozidi tani 2 nayo italipiwa kiingilio cha 25,000/- Tshs ukiweka VAT itakua 29,500/- Tshs. Ni muhimu sana uende na gari inayoeleweka, miundombinu mule ndani ni migumu kwa gari nyepesi. For my last trip I had two Landrovers, Discovery na Defender.

3. Malazi

Kitulo wana Bandas tatu ambazo kila moja ina rooms mbili, so watu sita wanaweza kulala katika hivyo vyumba sita ambavyo vina maji moto, duveti la maana na vingine vina kasebule fulani hivi kakujidai 🙂 Malazi kwa mswahili mwenzangu na mkaazi wa EA ni 29,500/- Tsh pekee

Hiki ni chumba ambacho mimi nililala,

Malazi kwa mtanzania ni 25,000/- tu

4. Matarajio

Wengi wanaenda Kitulo kwa matarajio ya MAUA, na msimu wa maua ni kati ya November hadi Aprili.

5. Chakula

Mgahawa rasmi haupo Kitulo, ili upate mgahawa inabidi uende kijijini Matamba, umbali wa kilomita 10 kutoka hifadhini. Lakini ukiwa na mpishi wako kama  unaweza kusafiri naye akakutengenezea msosi pale pale ndani ya hifadhi. Fahamu kuwa hao wapishi wako nao watalipia kiingilio na malazi pia.

Bahati nzuri, mhifadhi mmoja pale anatoa usaidizi wa chakula kwa wageni, anasaidia sana, Kwahiyo, ukiwasiliana naye mapema anaweza kukuandalia dishi kwa gharama isiyopungua 15,000/- (lunch/dinner) na 7,000/- kwa breakfast.

With arrangements anaweza kukuandalia lunch au breakfast katika hizo falls.

It is so lovely kwa kweli

6. Activities

Ni vema kwa mnaoenda Kitulo mkawa na activities, mfano hiking kwenye ziwa Dhambwe na Mafalls yake ikiwemo Nhumbe Falls, shamba la Ng’ombe wa Maziwa na mengine, wasiliana guide wako kwa ajili ya activities zaidi.

Pana Viewpoint moja nimeigundua trip hii, inapendeza sana, ila pana baridi isiyovumilika

Kawaida ukiwa hifadhini utatumia kilomita kama 50 hivi kufanya game drive, hivyo mbali na zile kilomita nilizotaja hapo juu unatakiwa uongeze na hizi. For a Discovery [injini ya V8 Supercharged] niliweka lita 60 (robo tatu ya tanki) na ikarejea na robo tanki nyumbani. For a Defender [300Tdi] huwa naweka lita 30 na narudi vizuri Mbeya mjini. Defender Puma, inabugia, itatumia full tanki takribani yote.

So, unaweza fanya haya makadirio. Landcruiser will accumulate even more 🙂 🙂

That’s all for today, natumai ipo elimu kwa anayependa Kitulo.

Nawatakia jioni njema

Makala hii imeandikwa na Shah Mjanja.

Shah Mjanja ni mpiga picha wa muda mrefu na muongoza wageni, Muandishi na Mtayarishaji wa makala za televisheni na filamu, Mhifadhi, Mwanamuziki na Msafiri. Ni muanzilishi wa Everyday Mbeya na Studio Native.

Shah Mjanja ni Ofisa wa Habari za klabu ya Mbeya City FC.

Tunawakaribisha wafanyabiashara na watoa huduma kufanya ushirika nasi kupitia kipindi chetu cha Utalii kinachoruka Jumamosi na Jumapili kupitia 100.9MHz redio Access FM. Kipindi chetu kinasikika mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Katavi, Songwe, Singida na Tabora.

Unaweza kushiriki nasi kama mdhamini.

Mawasiliano:

Ofisi: Posta House FL,
02 Posta Street, 53100 Mbeya
PO. Box 312 Mbeya

Simu: +255-682-326410
Barua Pepe: shah@everydaymbeya.com

ONYO: Picha zilizotumika katika makala haya zinamilikiwa kisheria na Studio Native na ni mali ya Studio Native, au/na washirika wake au za wamiliki wengine. Matumizi pasipo ruhusa au/na kwa lengo tofauti na mahudhui yaliyokusudiwa ni kinyume cha sheria na huenda ukawajibika. Usizitunze, kuzihamisha, kuzituma wala kuzitumia kamą kielelezo sememu yoyote kwa mfumo wa kielektroniki, machapisho au vyovyote vile.

Haya, basi sindikiza makala haya kwa kusikiliza kibao chao Les Wanyika kiitwacho Amigo 🙂