Njoo ujionee, ziwa lenye maajabu na utashangazwa zaidi na upekee wake. Si jengine, ni ziwa Ngosi. Je ni ipi asili ya neno ngosi? Neno Ngosi limetokana na neno la kisafwa “Ligosi” lenye maana ya “kubwa”
Huwenda ukawa unajiuliza masawali mengi kuhusu hili, ila everydaymbeya safaris tumekuja na suluhisho.
Kabla hatujaendelea let me give you an overview about Lake Ngozi.
- Ni ziwa la volcano la pili kwa ukubwa barani AFRIKA
- Its formation inakadiriwa kutokea 12,000years old ago
Ziwa hili ni la kipekee kwa upekee wake, limesheheni historia mbalimbali zikihusianishwa juu ya kutokea kwake. Historia hizo zenye mvuto wa aina yake hutoka kwa makabila mawili makubwa jiji mbeya, ambayo ni Wasafwa na Wanyakyusa.
SIFA ZA KIPEKEE
Picha ya ziwa Ngosi pamoja na ramani ya Africa.
Ziwa Ngosi lina sifa za kipekee ukiusianisha na maziwa yote duniani, sifa hizo ni
- LinabadiLika rangi na kua blue, kijani, nyeusi and sometimes linakua kama rangi ya maziwa.
- Kama huna bahati unaweza ukafika na usilione ziwa lenyewe. Hii husababishwa na hali ya hewa ya siku hiyo
- Kubwa kuliko ni ziwa lenye shape ya ramani ya Africa kukiwa na visiwa vyake vya unguja na pemba.
JE LINAPATIKA WAPI?
Lake Ngosi, linapatikana jijini mbeya, katika wilaya ya Rungwe, juu kabisa ya safu za mlima wa uporoto. Je ni ipi asili ya jina Uporoto? Uporoto limetokana na neno “Mporoto’’, Mporoto ni aina ya mmea ambao unapatikana kwa wingi katika msitu huo, kutokana na wingi wake ukapelekea eneo hilo kuitwa Uporoto.
Picha zikionesha mmea aina ya mporoto
JE UTALIFIKIAJE ZIWA NGOSI?
Ziwa Ngosi linapatikana juu ya mlima kabisa uitwao uporoto. Everyday Mbeya safaris tutakuchukua kutoka mbeya mjini, tayari kukupeleka katika ziwa ngosi. Zipo njia kuu mbili ambazo zitakufikisha kirahisi katika ziwa ngosi. Njia ya kwanza ni njia ya mchangani, ukipita katika njia hii utajifunza mambo mbalimbali ikiwepo mimea tiba. Hasara ya njia hii, hutaweza kuliona ziwa kwa ukubwa na uzuri wake. Njia ya pili ni njia ya iduda, njii hii utapata kuliona ziwa kwa ukubwa wake kabisa na manzari yake ya kuvutia.
JE NIKIPI UTENJOY UKIWA SAFARINI
Utaenjoy na kujionea manzari mazurii ya kuvutia, bila shaka hutatamani kushuka katika milima ya uporoto kutokana na hali ya hewa yake ya kuvutia.
Tarehe 31/9/2024, nilifanikisha kufika ziwa ngosi, ilikua ni weekend flani hivi ya kuvutia, kwani nilipata kuenjoy na kurefresh ma mind. Njiani kuelekea ziwa ngosi, nilipata kuenjoy mambo mbalimbali ikiwemo aibu ya miti. Najua unajiuliza ni ipi hiyo aibu ya miti, nisimalize uhondo, njoo everyday safari tukufikishe kilele cha uporoto ujioone mambo mbali mbali ya kuvutia
Pichani ni Mr. Everyday, katika eneo lenye miti inayoona aibu
NI ACTIVITIES GANI ZINAWEZA KUFANYIKA?
Activities mabli mbalimbali zinaweza kufanyika katika safari yako ya kuelekea lake ngosi, kama vile kupiga picha. Pia ni eneo zuri sana lenye utulivu ambalo unaweza kutulia wewe na familia yako, raki zako ama mpenzi wako na kuenjoy upepo mwanana utokanao na ziwa ngosi.
Kama upona stress ni eneo zuri sana lakuweza kutuliza stress kwani manzari yake ni mazuri na yenye utuluvu mkubwa.
Lakini pia kama ukihitaji kufanya kikao na mtu wako wa muhimu, ni eneo zuri sana ambalo unaweza kutulia na kujadili mipango yenu kaza wa waka
Yanini ugharamie fedha nyingi kwenda kumvisha mpenzi wako pete kwenye mahoteli ya kifahali, ikiwa lake ngosi ni eneo lenye utulivu mkubwa, chini ya usimamizi wa everyday safaris tukafanikisha jambo lako.
Wewe ambae unahitaji kufanya sherehe ya siku yako ya kuzaliwa, usihangaike, njoo everyday safari tuplan your trip to lake ngosi ukaenjoy na kufurahia siku yako pendwa kabisa.
Mambo mbalimbali yanaweza kufanyika, according to your wishes, welcome eveydaymbeya safaris tukuhudumie.
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI ZILIZOPIGWA KATIKA MOJA YA SAFARI ZA KUELEKEA LAKE NGOSI
Picha ikimuonesha Mr. Everyday (kulia), akiwa na mgeni wake (kushoto) ambe ni mwenyekiti mstaafu wa club ya mbeya city, katika moja ya viewpoint ya ziwa ngosi kupitia njia ya iduda, akimuelekeza mawili matatu kuhusiana na ziwa hili.
Picha ikimuonesha muongoza wageni Ali changae (wakwanza kulia), akiwa na wageni kuelekea Lake Ngosi.
Picha ikionesha miti inayoona aibu, ambayo inapatikana njiani kuelekea Lake Ngosi
Pichani ni Mr. everyday, muongoza wageni, mlinzi pamoja na wageni katika geti la hifadhi kupitia njia ya iduda, kuelekea lake ngosi.
Imeandaliwa na Kuandikwa;
Ali Changae, muongoza wageni kutoka everydaymbeya safaris, Pia ni mtaalam wa maswala ya utalii na Mali kale (Tourism and Cultural Heritage).
Kwa mawasiliano zaidi,
Tupigie Kwa namba +255682326410, pia tunapatikana ofisini kwetu, ofisi ipo mbeya mjini jengo la posta. Pia kwenye mitandao ya kijamii kama @everydaymbeya
Ofisi: Posta House FL,
02 Posta Street, 53100 Mbeya
PO. Box 312 Mbeya
auckland house painters
Great write-up, I’m regular visitor of one’s web site, maintain up the nice operate, and It’s going to be a regular visitor for a long time.