Unawakumbuka Uswahilini Matola? Kundi mashuhuri kutoka Mbeya Tanzania lililojivunia Soko Matola na rekodi kadhaa katika Bongo fleva ukiwemo Kosa la Marehemu?

Soko Matola, Mbeya Tanzania.

Licha ya kuwa mji huu unasemwa kuwa ni wa kale na kushuhudiwa na majengo ya enzi, bado kwa wakati wake ulikua mbele ya muda wake.

 

Tazama mpangilio wa kistaarabu wa majengo ya makazi na ofisi, pamoja na barabara zenye hadhi ya lami zinazoipa mitaa yake picha za kupendeza.

Katika picha ya hii unapaswa kuona jengo la Mkapa Conference Centre kati kati, kutokea hapo unaweza kugundua maeneo mengine mfano Chuo cha Utumishi wa umma, ghorofa la walimu na kota zake, hospitali ya Rufaa, chuo kikuu cha Dar, shule ya sekondari Loleza, kiwanja mpaka, na kadhalika.

 

Hapa Soko Matola ipo nyumba aliyowahi kuishi Mzee Nyerere Baba wa Taifa letu, ilikua nyumba ya Binti Zaituni, na masimulizi yanasema wazee wengi waliopigania uhuru walifika katika nyumba hiyo, mfano Mzee Mandela, Mzee Mugabe na wengine. Ilikua nyumba ya vikao vya ukombozi wa Afrika dhidi ya mabavu ya wakoloni.

 

 

 

Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu Mbeya katika www.everydaymbeya.com Pia, kwa picha zaidi fuatilia ukurasa wetu rasmi wa Instagram kwa anuani hii (@everydaymbeya). Iwapo utashirikisha picha za Everyday au wakati wa Everyday usisahau kuhashtag #everydaymbeya.

Makala hii imeandikwa na Shah Mjanja.

Shah Mjanja ni mpiga picha wa muda mrefu, Muandishi na Mtayarishaji wa makala za televisheni na filamu, Mhifadhi, Mwanamuziki na Msafiri. Ni muanzilishi wa Everyday Mbeya na Studio Native.

Shah Mjanja ni Ofisa wa Habari za klabu ya Mbeya City FC.

Mawasiliano:

Simu: +255-682-326410
Barua Pepe: shah@everydaymbeya.com