Hello Everyday,
Licha ya kuwa ziwa Ngosi is one of the best hike in the world bado taarifa sahihi za safari kuelekea ziwani Ngosi ni chache, hivyo kwa umuhimu wake ninakuandikia makala haya ili yaweze kukusaidia kulifikia; ukiwa mwenyewe au na tour guide.


Geti la hifadhi

Kabla hatujaanza kutazama taarifa zake za safari let me tell you something about the lake japo kwa uchache…

Facts

  • Ziwa Ngosi ni ziwa la volkano la pili kwa ukubwa Afrika
  • Limejipamba kwa ramani ya Afrika
  • Lina urefu wa kilomita 2.5 na kina chenye mita 74

So here is the list of what you should know before going to lake Ngosi!

1. TIME

Licha ya kuwa unaweza kwenda ziwani muda wowote, fahamu kuwa muda mzuri zaidi wa kwenda ziwani huanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa mbili asubuhi.

Kwanini asubuhi?

Kutokana na hali hewa ya msitu wa Uporoto mara nyingi mvua huanza kunyesha walau kuanzia saa sita mchana, hivyo ukianza safari  yako mapema itakupa muda mzuri wa kukwepa mvua na kupata the most of lake Ngosi experience bila mashaka.

Nani hapendi clear blue skies?


Msitu wa Uporoto

Kawaida, sisi Everyday Mbeya huweka mipangilio ya safari kutoka hotelini au hapo ulipo kuanzia saa moja asubuhi, wastani wa takribani dakika 30 zinatosha kutoka Mbeya mjini hadi geti la hifadhi, na kutoka geti la hifadhi hadi ziwani ni hike ya dakika 30 tu, hivyo ni matarajio kuwa walau saa tatu asubuhi mgeni atakua tayari ameishafika ziwani.

Vilevile, hali ya hewa kadiri muda unavyokwenda huleta FOG (Ukungu) ambao hulifunika ziwa, ni muhimu kuwahi ili kufurahia mandhari ya ziwa.

Video hii hapa chini inaonesha mabadiliko ya hali hewa ziwani na wakati fulani ziwa lote hufunikwa kabisa na kushindwa kuonekana.

Mara nyingi wageni wetu wamefika ziwani na kurudi bila kuona ziwa, isn’t it an adventure?

Tahadhari: Ni vema iwapo utachukua muamvuli ili mvua ikinyesha upate kujisitiri.

2. Nguo
Nimeona watu wakienda ziwani na nguo nyepesi, na wakafurahia, ukweli ni kuwa going to the lake need a bit of physical exercises kutokana na miinuko mikali, lakini wakati wote ukiwa na nguo itakayofunika mwili wako itakuondolea karaha wakati wa kutembea msituni.

Kwanini ujivike kwa mavazi yanayofaa?

– Mbung’o (Tse-Tse Flies).
Msitu wa Uporoto unawavutia wadudu ambao huwa ni taabu mno njiani, ukiwa na nguo iliyokusitiri zaidi huwa nafuu kwa msafiri.

– Tope na Utelezi.
Si jambo la kushangaza msafiri akiteleza njiani wakati wa kupandisha au kushuka, hivyo nguo isiyo nyepesi huweza kukupunguzia makali ya maumivu pale utakapo-teleza na kuanguka.

Wakati fulani kushuka katika crater lilipo ziwa huenda ikahitaji kutambaa kwa kutumia makalio yako, basi nguo imara ni muhimu zaidi. Tazama zaidi video hii kujionea mambo.

3. Viatu

Successful hiking yoyote inahitaji uwe mwepesi, like a super car -uzito ni adui wa mwendo; lakini unahitaji umakini katika kuchagua ni viatu gani upandishe navyo ziwa Ngosi. Ndio maana hata watengenezaji wa gari za mwendo kasi hutumia malighafi zilizo nyepesi lakini imara. Safari boots… Yes zinafaa lakini zisiwe nzito zaidi!


Raba nyepesi zenye kashata/soli imara vinafaa zaidi.

Viatu imara ni silaha muhimu katika njia za kuelekea ziwani, zinatakusaidia usiteleze lakini pia kama hazipitishi maji basi zitakufaa sana pale mvua itaponyesha au utakapopita mahala penye matope au unyevu.

Vipo vizingiti vingi njiani, mfano magogo ya miti iliyoanguka, majani, matope na hata wadudu mfano wa siafu. Ukiwa na viatu imara huwa ni nafuu sana kwako. Baadhi ya sehemu njiani zimezuiliwa kwa miti iliyodondoka na utahitaji kuivuka kwa miguu yako.

4. Usafiri

Mamlaka ya hifadhi chini ya TFS inafanya kazi kubwa mno kurekebisha miundombinu kuelekea ziwani, lakini zipo sehemu au upo wakati kutokana na mvua huenda barabara ikawa na changamoto. Hii ndio sababu ili ufike hifadhini utahitaji a serious 4×4.


Wageni wetu katika ‘pozi’ mbele ya Landrover Defender


Guide wetu Lusajo akisawazisha njia wakati wa safari

Tofauti na siku za nyuma kwa sasa miundombinu kwa sehemu kubwa inaruhusu gari ndogo kufika, licha ya changamoto chache njiani lakini tumegundua kwa sehemu kubwa gari ndogo hata isiyo na four-wheel system inaweza kufika au tuseme kujaribu kufika jirani na geti la hifadhi.

Kongole sana kwa serikali ya watu wa Tanzania kupitia wakala wa huduma za misitu kwa maboresho makubwa wanayofanya hapa ziwa Ngosi.

Kwanini ufike geti la hifadhi?

Mfano, umbali wa kutoka kituo cha basi hapo kituoni Iduda/magorofani hadi kufika geti la hifadhi pana urefu wa kilomita 7.2, ukiweza kusafiri umbali huu kwa gari itakusaidia kutembea kilomita 2.5 zilizosalia ndani ya hifadhi. Fahamu kuwa hakuna barabara ya gari ndani ya hifadhi.

Si gari zote zinaweza kupita katika barabara hii ya kilomita 7.2 kutokana na miinuko mikali, mabonde na utelezi.


Nissan Dualis njiani kuelekea ziwa Ngosi

Kwanini tunahitaji gari kwenda ziwa Ngosi?

Going to lake Ngosi does not really need a car, mfano wako wasafiri ambao hawataki kwenda ziwani kwa magari, wao wanataka kutembea kutokea barabarani [Magorofani/Iduda] hadi ziwani. Wasafiri wengine wanataka kutembea zaidi kuliko kutumia gari. Kutegemea na malengo ya msafiri, wapo wanaopenda hiking lakini wapo wachache ambao wao hutaka kwenda kutalii kwa luxury pasi na bughuza.


Mgeni wetu Mr. Eric na Guide wetu James

Mr. Eric ni mmojawapo wa wapandaji milima mashuhuri duniani, anazo rekodi tele huko New Mexico, alipokuja alihitaji kutembea kutoka mjini hadi ziwa Ngosi, na safari yetu ya kutembea ilianzia Hill view hoteli, teena kwa kukimbia. Fikiria…

Kwahiyo, si muda wote gari ina umuhimu.


Msafiri anaweza pia kutumia pikipiki kuelekea geti la hifadhi

5. First Aid Kit

Mahala popote first aid kit ni lazima na hasa wakati wa safari…


Hawa ni wageni wetu kutoka UnZip Tanzania, mmoja wa wageni hawa alitegua mguu baada ya kuteleza msituni, uwepo wa first-aid kit ulisaidia kumpatia matibabu ya awali.


Hii ni repellent muhimu sana kuelekea ziwani, inasaidia kuwafukuza wadudu, ni muhimu iwepo katika sanduku lako la dharura au mkoba wako wa safari

6. Usalama

Hauhitaji askari ili kwenda ziwani, msitu hauna wanyama hatarishi zaidi ya mabata, nyani na vicheche. Siku za kale palikuwepo na majangili wa mbao kutoka katika miti iliyopo msituni, lakini kwa sasa hakuna kabisa. Hatahivyo, si hekima kwenda ziwani Ngosi ukiwa mwenyewe na inashauriwa uwe na muongoza wageni au mwenyeji.


Mgeni wetu Maria kutoka Chicago huko Amerika akisindikizwa na askari wa hifadhi

Hifadhi imeweka maafisa wakiwemo askari na raia ambao kazi yao ni kusimamia shughuli ziwani lakini pamoja na kukusanya mapato. Watoa huduma hao wanaweza kukusaidia kufika ziwani vilevile.

7. Chakula

Hakuna mgahawa ukiwa ziwa Ngosi, Everyday Mbeya huandaa chakula katika lunch-box kwa kila msafiri. Tunashauri walau lita moja ya maji na vyakula vyepesi.

8. Viingilio

Ni sharti kwa kila mgeni kulipia ada za viingilio unapotaka kuingia katika hifadhi ya msitu wa Uporoto lilipo ziwa Ngosi, mamlaka hutoza 2,000/- Tshs kwa mzawa au raia wa jumuiya ya East Africa na dola 10 za marekani kwa mgeni asiye raia wa jamuhuri yetu.

Wageni wenye kibali cha makazi wanatozwa dola 05 za marekani, na watoto  watanzania wasiozidi miaka kumi na saba watalipia Tsk 1,000/-, watoto wa kigeni watalipa dola 05 za marekani.


Mgeni wetu Kelvin Pam akifurahia mandhari ya ziwa Ngosi, Kelvin ni mshindi wa kwanza wa Big Brother Africa kutoka Nigeria


Viewpoint ya ziwa Ngosi

9. Njia

Zipo njia zaidi ya moja zinazoweza kukufikisha ziwa Ngosi, leo nitakueleza njia mbili muhimu zaidi

Mchangani Trail

Njia hii ni ile inayoingilia geti la mchangani umbali wa kilomita 33 kutokea Mbeya mjini. Njia hii ipo mbele kidogo baada ya kituo maarufu cha ‘namba wani’ katika barbara ya Tanzania Malawi.


Wageni wetu katika picha ya pamoja kituoni mchangani


Wageni wetu Mariam na Jolyne wakipandisha ziwani na guide wetu Mwakasungula kupitia njia ya mchangani


Wageni wetu wakishuka katika crater ya ziwa Ngosi kupitia njia ya mchangani

Iduda Trail

Hii ni njia inayotumiwa na wengi, ipo wastani wa kilomita 12 kutokea Mbeya Mjini, inapita kijijini Iduda kupitia magorofani. Hii ni njia inayoshauriwa sana na wahifadhi.


Muonekano wa ziwa kutokea njia ya Iduda


Mgeni wetu akishauriana jambo na guide

Briefing katika geti la hifadhi kabla ya safari
  • Mchangani Trail
    +Ina miti/mimea zaidi hivyo hufaa kwa tafiti za dawa/mitishamba
    +Ni rahisi kushuka chini ya crater kwa njia hii
    -Hutoweza kuliona ziwa lote
    -Umbali mrefu kutokea Mbeya mjini [33km]
    -Njia ya kutembea ndani ya hifadhi ni ngumu na mbaya [Inafaa kwa wanaopenda Extreme Hiking]
  • Iduda Trail
    +Muonekano mzuri wa ziwa lote
    +Jirani na Mbeya mjini
    +Njia ya kutembea ndani ya hifadhi ina nafuu
    -Si rahisi kushuka chini ya crater
    -Wadudu wengi njiani [Siafu na Mbung’o]

Mara zote jaribu kushauriana na muongoza wageni wako kuhusu njia unayohitaji kutumia kulingana na malengo yako, lakini pia ni muhimu kumueleza mwenyeji wako kuhusu hali yako ya kimwili ili aweze kukushauri njia sahihi ya kwenda ziwa Ngosi. Furaha yetu ni kukusaidia wewe kufika ziwani, hivyo ni muhimu kupata taarifa sahihi za hali yako ya afya na malengo yako ya safari.

Muonekano wa ziwa Ngosi kutokea viewpoint ya Iduda huwavutia wasafiri wengi wanaotembela ziwa Ngosi, na wengi hao huridhika kutazama ziwa kutokea hapo, lakini watoa huduma wetu wanaweza kukupeleka chini ya crater lilipo ziwa na ukaweza kugusa maji yake.

Huhitaji kuwa na misuli ili ufike ziwa ngosi, tofauti na watu wengi wanavyozungumza -mtu yeyote anaweza kufika ziwani. Tofauti ni kuwa, kulingana na hali ya mwili wako kuna wengine hutembea kwa muda mchache na wengine zaidi.


Mgeni wetu Hashim Ibwe kutoka Azam TV

Licha ya kuwa njia zote zinakufikisha katika ziwa, sisi tunashauri utumie njia ya iduda ambayo ni rahisi na jirani na Mbeya mjini, lakini pia ni nafuu kwa gharama za safari pamoja na ubora wa muonekano.


Muonekano kutokea viewpoint ya Iduda


Muonekano kutokea viewpoint ya Mchangani

10. Maji ya Ziwa

Maji ya ziwa Ngosi yanatokana na chemichemi zilizo chini yake, ni maji ya kawaida kama yalivyo maji mengine. Licha ya kuwa wakaazi wa eneo jirani wanayo imani kuwa maji hayo yanaondoa mikosi na nuksi, hakuna aliyewahi kuthibitisha hilo hadi wakati huu.

Huenda yakawa si maji salama kwa kunywa kutokana na ukweli kuwa yamekaa hapo kwa muda mrefu. Maji yake yana harufu kiasi na mapovu kutokana na joto linalotoka chini.

Kwa hali hii hatushauri kuogelea katika maji ya ziwa Ngosi wala kuyanywa.


Wageni wetu katika picha ya pamoja kupitia njia ya mchangani


Wageni wetu katika picha ya pamoja kupitia njia ya mchangani

Bila shaka chapisho hili limekupatia taarifa muhimu zitakazokusaidia kufika ziwa Ngosi, kama vile Hitoshi ninakuwekea hapa chini video inayoonesha safari ya kuelekea ziwani kwa ujumla wake. Enjoy!

Wasalaam,

Makala hii imeandikwa na Shah Mjanja. Shah Mjanja ni mpiga picha wa muda mrefu, muandishi na mtayarishaji wa makala za televisheni na filamu, mhifadhi, mwanamuziki na msafiri. Ni muanzilishi wa Everyday Mbeya na Studio Native.

Shah Mjanja ni Ofisa wa Habari za klabu ya Mbeya City FC.

Mawasiliano:

Simu: +255-682-326410
Barua Pepe: shah@everydaymbeya.com

Work Address
Posta House, FL
Posta Street/Lupaway road
Box 312
Mbeya Town